Sunday 27th of April 2025

Available Translations

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

Sabbihisma Rabbikal A'laa

Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,

Surah Number : 87 , Ayat Number : 1

"الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ"

Allazee khalaqa fasawwaa

Aliye umba, na akaweka sawa,

Surah Number : 87 , Ayat Number : 2

"وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ"

Wallazee qaddara fahadaa

Na ambaye amekadiria na akaongoa,

Surah Number : 87 , Ayat Number : 3

"وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ"

Wallazeee akhrajal mar'aa

Na aliye otesha malisho,

Surah Number : 87 , Ayat Number : 4

"فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ"

Faja'alahoo ghusaaa'an ahwaa

Kisha akayafanya makavu, meusi.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 5

"سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنْسَىٰ"

Sanuqri'uka falaa tansaaa

Tutakusomesha wala hutasahau,

Surah Number : 87 , Ayat Number : 6

"إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ"

Illaa maa shaaa'al laah; innahoo ya'lamul jahra wa maa yakhfaa

Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 7

"وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ"

Wa nu-yassiruka lilyusraa

Na tutakusahilishia yawe mepesi.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 8

"فَذَكِّرْ إِنْ نَفَعَتِ الذِّكْرَىٰ"

Fazakkir in nafa'atizzikraa

Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 9

"سَيَذَّكَّرُ مَنْ يَخْشَىٰ"

Sa yazzakkaru maiyakhshaa

Atakumbuka mwenye kuogopa.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 10

"وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى"

Wa yatajannabuhal ashqaa

Na atajitenga mbali nayo mpotovu,

Surah Number : 87 , Ayat Number : 11

"الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ"

Allazee yaslan Naaral kubraa

Ambaye atauingia Moto mkubwa.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 12

"ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ"

Summa laa yamootu feehaa wa laa yahyaa

Tena humo hatakufa wala hawi hai.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 13

"قَدْ أَفْلَحَ مَنْ تَزَكَّىٰ"

Qad aflaha man tazakkaa

Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 14

"وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ"

Wa zakaras ma Rabbihee fasallaa

Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 15

"بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا"

Bal tu'siroonal hayaatad dunyaa

Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!

Surah Number : 87 , Ayat Number : 16

"وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ"

Wal Aakhiratu khairunw wa abqaa

Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 17

"إِنَّ هَٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ"

Inna haazaa lafis suhu fil oolaa

Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,

Surah Number : 87 , Ayat Number : 18

"صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ"

Suhufi Ibraaheema wa Moosaa

Vitabu vya Ibrahimu na Musa.

Surah Number : 87 , Ayat Number : 19

Surah Arabic Ayat , Audio and Translations

Listen Surah Al-Ala